Polisi Kenya wanamsaka Mtanzania aliyeua kisa ugali

0
64

Polisi nchini Kenya wanamsaka Mtanzania anayeshukiwa kumdunga kisu mwenzake katika eneo la uchimbaji dhahabu huko Narok nchini Kenya kisa kikidaiwa ni bakuli la ugali.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Narok, Kizito Mutoro amesema wanaume hao wawili walikuwa wakipata mlo wa jioni baada ya kutwa nzima katika migodi ya Got Kabong huko Transmara Magharibi siku ya tukio hilo lilipotokea.

“Iliripotiwa kuwa walipokuwa wakila chakula, mzozo ulitokea kati ya Bw. Mungare Busene (27), na mwingine aliyemtambulika kwa jina la Magige (23), (wote Watanzania) kuhusu ugali waliokuwa wakila,” amesema Kamanda.

Mtanzania afariki kwa Ebola nchini Uganda

Inaaminika kuwa Busene alichukua kisu cha jikoni na kumchoma Magige kwenye mguu wa kushoto, na kumsababishia jeraha kubwa sana na kukimbizwa katika Hospitali ya Lolgorian Level Four ambapo baadaye alitangazwa amefariki.

Inadaiwa baada ya shambulio hilo, mtuhumiwa alienda mafichoni kuepuka mkono wa sheria, na kwa sasa Polisi wanachunguza tukio hilo na pia wanamsaka mshukiwa huyo.

Send this to a friend