Polisi kuchunguza kupotea kwa Mjumbe wa Sektetarieti CHADEMA

0
63

Jeshi la Polisi Tanzania limesema linafuatilia taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Ally Mohamed Kibao alichukuliwa na watu wasiojulikana akiwa safarini ndani ya basi la Tashrif eneo la Tegeta, Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema baada ya kusikia taarifa hizo kupitia vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, lilipokea taarifa hiyo na kuanza uchunguzi wake.

“Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa, lilipokea taarifa hiyo na kuanza uchunguzi wa kubaini kilichotokea, chanzo chake na watu waliohusika ni akina nani,” imeeleza taarifa ya Jeshi la Polisi.

Mapema leo, Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika alieleza kuwa Ally Kibao ambaye ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama Taifa, alishushwa na watu waliokuwa na silaha na kuanza kumpiga kisha kuondoka naye, na kwa sasa juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Send this to a friend