
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linaendelea kuchunguza mauaji ya watu wawili ambao wamejulikana kwa majina ya Mashua Bakari (35) na Salha Halfan (22) wote wakazi w Taliani Chanika, Dar es Salaam.
Taarifa ya Polisi imesema tukio hilo linadaiwa kutokea Septemba 25, 2025 asubuhi, ambapo miili ya wahusika hao ilikutwa ndani ya chumba cha kupanga alichokuwa akiishi mwanamke huyo ikiwa na majeraha baada ya kudaiwa mwanaume kumjeruhi mwanamke na baadaye kujijeruhi kwa kitu chenye ncha kali, kisha wote wawili kupoteza maisha.
Aidha, taarifa hiyo imesema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi na mzozo mkubwa ulioibuka kati yao.






