Polisi kuwasaka waliomteka na kumjeruhi mfanyabiashara Sativa

0
62

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limesema limeanza uchunguzi na kuwasaka watu wote waliohusika na kutekwa kwa mfanyabiashara aitwaye Edgar Mwakabela (27) maarufu Sativa ambaye alitoweka jijini Dar es Salaam Juni 23, mwaka huu na kupatikana usiku wa kuamkia Juni 27, 2024.

Kaatika taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Kaster Ngonyani amesema Kijana huyo ambaye amepatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Mlele mkoani Katavi akiwa na majeraha amelazwa katika hospitali Mpimbwe Kibaoni kwaajili ya matibabu.

“Amepatikana leo nadhani video clip mmeiona ile clip inajielezea vizuri, na sisi tumemuona ila sasa hivi haongei, anaongea kwa tabu sababu ya hizo dawa, nguo zake hazijaloana damu, damu zipo kichwani, tunaendelea kuwatafuta wote waliomfanyia tukio hilo, Daktari atatupa taarifa ameumia sehemu gani na kitu kilichomchoma ila uchunguzi wa kuwatafuta waliofanya tukio hilo unaendelea,” amesema.