
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limesema Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu anashikiliwa kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi.
Akizungumza na Swahili Times kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Marco Chilya amesema mpaka sasa hakuna kiongozi yeyote wa CHADEMA anayeshikiliwa zaidi ya Mwenyekiti Lissu.
“Mpaka sasa hakuna aliyeshikiliwa ila naona wanatafuta kushikiliwa, naona kuna kitu wanakaidi lakini bado hawajashikiliwa,” amesema Kamanda.
Aidha, amesema taratibu zote zitakapokamilika Mwenyekitu Tundu Lissu atafikishwa mahakamani.