Polisi: Madereva watembee na vyeti vya udereva, tutavikagua

0
55

Katika mchakato wa uhakiki wa leseni za madereva, Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litawachukulia hatua kali madereva na shule za udereva zitakazobainika kuuza na kununua vyeti vya udereva.

Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Deus Sokoni amesema katika mchakato huo wa ukaguzi, dereva anapaswa kuonesha leseni pamoja na cheti cha udereva alichokipata kutoka katika chuo cha udereva alichosomea.

“Tutoe rai kwa wale wamiliki wa shule za udereva kutokuuza vyeti, ukienda shule ukapewa cheti bahati nzuri tukaingia kwenye database [kanzidata] tukagundua umenunua cheti na shule tunafunga, haitakuwa na nafasi tena, kwa hiyo tunataka uingie darasani usome ili uzijue sheria, ujue matumizi sahihi ya barabara,” amesema.

Terminal II ya Uwanja wa Ndege Dar es Salaam kufungwa kwa miaka miwili

Ameongeza, “huwezi kupata leseni bila kusoma, msingi wa kisheria unasema ili upate leseni ya kuendesha gari yoyote duniani lazima uingie darasani, kwa hiyo leseni ni matokeo ya wewe kwenda darasani ukajifunza katika shule zilizosajiliwa.”

Aidha, Sokoni amesema vyuo vyote vilivyosajiliwa viko katika mfumo wa leseni za udereva Tanzania, hivyo ikiwa dereva hatokuwa na cheti chake wakati wa ukaguzi itamlazimu kutaja chuo husika kisha wataangalia kwenye mfumo endapo kimesajiliwa.

Send this to a friend