Polisi: Marufuku kuvaa nguo zinazofanana na sare za majeshi 

0
84

Jeshi la Polisi limewaonya baadhi ya watu, kampuni binafsi za ulinzi na baadhi ya walinzi wa viongozi wenye tabia ya kuvaa mavazi yanayofanana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama.

Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema Sheria ya Kanuni ya Adhabu inakataza mtu yeyote ambaye si askari wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa sare za majeshi.

Aidha, Jeshi la Polisi limewataka wale wote wenye tabia ya kuvaa mavazi yanayofanana na sare za majeshi kinyume na sheria za nchi, kuacha tabia hiyo mara moja kwani jeshi halitasita kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Jeshi limetoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuendelee kuiweka nchi salama.

Send this to a friend