Polisi: Mtoto atakayepotea kipinidi cha sikukuu, mzazi atachukuliwa hatua

0
18

Jeshi la Polisi limetangaza kuwa kuanzia hivi sasa, mtoto yeyote atakayepotea, kunyanyasika au kutokuwa na usimamizi katika kipindi hiki cha sikukuu, mzazi wa mtoto huyo atachukuliwa hatua.

Akizungumza Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam, amewataka wazazi kuhakikisha usalama wa watoto wao pindi wanapokwenda kwenye matembezi katika sikukuu zinazokuja hivi karibuni.

Daktari: Mwanaume akiingia leba inamsaidia mkewe kujifungua salama

“Imezoeleka kwenye sikukuu kuwa na matukio ya watoto kupotea na kuletwa katika vituo vyetu vya polisi, wakati mwingine watoto wanakaa vituoni hadi saa nane na wengine wakinyanyasika kwa kukosa usimamizi thabiti. Sasa hatutoacha hili liendelee, tutachukua hatua za kisheria,” amesema.

Aidha, ameshauri wazazi na walezi kuacha kuegemea upande mmoja wa kuwapeleka kwenye matembezi watoto wao, badala yake watumie muda huo kuwapeleka kwenye nyumba za ibada ili wamjue Mungu na kuwa na maadili mema.

Send this to a friend