Polisi Tanga wapewa rungu dhidi ya wanawake wanaojiuza

0
91

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha biashara ya madanguro maarufu kama madada poa inakoma mara moja jijini Tanga.

Mganndilwa ametoa agizo hilo wakati wa  kikao cha cha baraza la madiwani wa Halamashauri ya Jiji la Tanga ambapo aliyataja maeneo hayo kuwa ni  Sabasaba na Barabara ya Uhuru na kusema kuwa  wanaofanya biashara kwenye maeneo hayo watafute miji mingine.

“Kuna maeneo kwetu sisi bado kuna, madanguro ambayo dada zetu wanajiuza naomba nitumie hadhara hii kwa kuwa vyombo vya dola vipo hapa niwaombe tuanze kushughulika na hawa watu natamani tuone mji wetu unakuwa safi hatutaki kuona hizi biashara za kujiuza jeshi la polisi wakati nikifanya operesheni zenu basi mshughulike na watu hawa,” amesistiza.

Katika hatua nyingine Mgandilwa amesema pamoja na hayo analipongeza jiji hilo kwa kuweza kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi na kutaka kuwalipa fidia wananchi ambao bado wana migogoro ya fidia zao lengo ni kuondokana na migogoro isiyokuwa na lazima.

Send this to a friend