Polisi: Tunafanya uchunguzi taarifa mpya kupotea kwa aliyekuwa mgombea udiwani CCM

0
123

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tarime Rorya limethibitisha kuanza uchunguzi kuhusu video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikihusishwa na kupotea kwa mgombea udiwani wa CCM Kata ya Sirari, Sinda Samson Mseti.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, video hiyo inaonyesha kundi la watu wakiingia katika nyumba moja usiku, ambapo inadaiwa kuwa Agosti 11, 2025 saa nane usiku, watu hao walimkamata ndugu wa mwenye nyumba hiyo, Sinda Mseti, ambaye alikuwa mgombea udiwani wa CCM.

“Imeeleza kuwa watu hao ndio waliomteka Sinda Mseti, ambaye taarifa zake zilifikishwa Polisi na kudai kuwa Agosti 08, 2025 alikamatwa na kuchukuliwa na watu waliokuwa wanatumia gari lenye usajili wa namba za nchi jirani,” imeeleza.

Imeongeza kuwa ” Taarifa iliyotolewa Agosti 06, 2025, Jeshi la Polisi Mkoa wa Tarime Rorya lilikuwa linaendelea na uchunguzi wake, hivyo kwa taarifa hii mpya limeanza pia uchunguzi wake hadi ukweli utakapojulikana.”

Hata hivyo, jeshi limesema linaendelea kutoa wito kwa mwenye taarifa za kweli kuziwasilisha kituoni ili zifanyiwe kazi hadi atakapopatikana Sinda  Mseti.

Send this to a friend