Polisi: Tunawasaka bodaboda waliochoma basi Tanga

0
46

Jeshi la Polisi limesema linaendelea kuwasaka waendesha pikipiki maarufu bodaboda waliohusika kuchoma basi la kampuni ya Sai Baba Express katika Kata ya Mtonga, Halmashauri ya wilaya ya Korogwe baada ya mwenzao kugongwa na basi hilo ili waweze kufikishwa mahakamani.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema kitendo cha kuchoma moto basi hilo ni kudhulumu haki za watu wengine ambao hawakuhusika na tukio la ajali, kwani mali za abiria zimeteketea kwa moto na kuwaingiza katika hasara kubwa.

“Jeshi la polisi linatoa wito kwa bodaboda wenye tabia kama hizo wajitafakari, waelimishane na wajiulize; je sisi nasi tunafuata sheria za usalama barabarani? Halikadhalika, wajiulize; na sisi tunavyovunja sheria za usalama barabarani je, pikipiki zetu nazo zichomwe moto? Ni wazi kwamba jibu ni hapana na si sahihi mbele ya sheria,” amesema.

Aidha, jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi kuacha tabia hiyo kwakuwa ni kinyumbe na sheria na inakiuka haki za binadamu.

Send this to a friend