
Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limesema linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta wale wote waliopanga, kuratibu na walioshiriki kuharibu mali za umma na za watu binafsi katika maeneo mbalimbali nchini Oktoba 29, 2025.
Aidha, limetangaza kuwa linawasaka Josephat Gwajima, Brenda Rupia, John Mnyika, Godbless Lema, Machuku Kadutu, Deogratius Mahinyila, Boniface Jacob, Hilda Newton, Award Kalonga na Amaan Golugwa huku likiwataka wajisalimishe mara moja.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limesema hatua za kisheria kwawahalifu ambao tayari wamekamatwa zinaendelea kote nchini na baadhi tayari wamefikishwa mahakamani.
Hata hivyo, Jeshi hilo limetoa onyo kwa mtu au kikundi kinachopanga kufanya uhalifu kwa namna yoyote, likisema kuwa halitasita kuchukua hatua.








