Polisi: Tunawasaka waliozusha taarifa za mauaji ya raia wa Kihindi

0
44

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii kuwa kuna raia watatu wenye asili ya India wameuawa na kutupwa kwenye ufukwe wa Bahari eneo la Kigamboni, na kwamba litawakamata watu wote walioanzisha taarifa hizo.

Kamanda wa Polisi, Jumanne Muliro amesema taarifa hizo zimekuja baada ya watu wawili kukamatwa Februari 2 mwaka huu kwa tuhuma za mauaji ya mtu mmoja aliyepatikana katika ufukwe Kigamboni baada ya ndugu zake kudai kuwa mtu huyo alitekwa.

Mahakama yabariki kuuawa aliyeua mtoto kisa alimrushia mawe

“Jeshi la Polisi linafuatilia na halikubaliani na tabia hii ambayo inaelekea kuwa sugu na linafuatilia kwa karibu, litawakamata kuwahoji walioanzisha taarifa hizi za uongo na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa

Ameongeza kuwa hali ya Dar es Salaam ni shwari na polisi wanaendelea na upelelezi juu ya tukio la mauaji ya mtu huyo, hivyo taarifa zaidi za kisheria zitatolewa pindi uchunguzi utakapokamilika.

Send this to a friend