Polisi: Tutawakamata waliojaribu kumkamata kwa nguvu mfanyabiashara

0
46

Jeshi la Polisi nchini limesema litawakamata watu walioonekana kwenye picha mjongeo wakijaribu kumkamata na kujaribu kumwingiza kwenye gari kwa nguvu Deogratius Tarimo, mfanyabiashara na mkazi wa Kibaha mkoani Pwani.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Polisi, DCP David Misime ambapo imeeleza kuwa tukio hilo liliripotiwa na mfanyabiashara huyo katika kituo cha Polisi Gogoni jijini Dar es Salaam Novemba 11, mwaka huu.

“Kulingana na ushahidi uliowasilishwa kituoni hapo na yeye mwenyewe ni kwamba chanzo cha tukio na kilichomsukuma kufika katika hoteli ya Rovenpic iliyopo eneo la Kiluvya jijini Dar es Salaam ni kufanya mazungumzo ya biashara ambayo amekuwa akiwasiliana kuifanya na aliokuwa anawasiliana nao toka Oktoba 25, 2024,” imeeleza taarifa.

Aidha, Jeshi la Polisi limesema linaendelea kukusanya ushahidi ili hatua zingine ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria kwani hakuna aliye juu ya sheria.

Send this to a friend