
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limesema linachunguza taarifa ya kutoonekana kwa Mtawa, Silianus Balyalemwa Korongo (49) ambaye ametoweka kutoka kwenye nyumba ya malezi ya Watawa wa Shirika la Ndugu Wadogo wa Franciscan tangu Desemba 01, 2025.
Taarifa zimeeleza kuwa mara ya mwisho Mtawa huyo alikwenda kununua vifaa vya ujenzi na hakurejea tena.
Aidha, Polisi wametoa rai kwa mwananchi yeyote mwenye taarifa zozote kuhusiana na kutoweka kwa Mtawa huyo aziwasilishe kituo chochote cha Polisi ili zisaidie uchunguzi.








