
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limeanza uchunguzi kufuatia tuhuma zinazohusisha baadhi ya viongozi wa kisiasa wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, wanaodaiwa kupita mitaani na kuwalaghai wananchi kukusanya na kuandika namba zao za vitambulisho vya kupigia kura.
Polisi wamesema kwamba, endapo uchunguzi uthibitisha tuhuma hizo, wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha, Jeshi la Polisi limewataka wananchi wa Kigoma kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na limeahidi kuhakikisha taratibu za kisheria zinafuatwa kikamilifu.








