Polisi wachunguza bilioni 6 zilizoingizwa kwenye akaunti za THRDC

0
42

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amesema kuwa jeshi hilo linashikilia akaunti za benki za Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kuchunguza kiasi cha fedha TZS 6 bilioni zilizoingizwa kwenye akaunti zao.

Sirro amesema lengo ni kutaka kubaini endapo fedha hizo ni halali au la, na kama ni hali, ifahamime zimelenga kutumika katika shughuli gani.

Hivi karibuni THRDC ilitangaza kusitisha shughuli zake nchini Tanzania baada ya akaunti zake katika Benki ya CRDB kufungwa kwa maelezo kuwa hawajawasilisha mkataba kati yao na wafadhili katika Ofisi ya Hazina na Ofisi ya Msajili.

Send this to a friend