Polisi wadaiwa kuzuia kuingia na simu kesi Mbowe

0
27

Wakati upande wa Jamhuri ukiendelea kutoa ushahidi wake katika kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake watatu, mvutano umeibuka katika geti la kuingia Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi baada ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA, waandishi wa haabri na watu wengine kuzuiwa kuingia.

Katika mvutano huo, aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob (CHADEMA) amehoji sababu za polisi kuwazuia kuingia wakati siku zote wamekuwa wakiingia kwa kufuata taratibu na hakuna vurugu au uvunjifu wa amani uliotokea.

“Nimetaarifiwa kwamba Polisi na/au Mahakama wanazuia watu kuingia na simu mahakamani ili kudhibiti utoaji wa taarifa za yanayoendelea kwenye kesi ya uongo dhidi ya Mwenyekiti Mbowe. Haki lazima ifanyike na ionekane imefanyika. Haki haiwezi kufanyika gizani na ikaonekana imefanyika,” ameandika Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu lissu

Baada ya mvutano kuwa mkubwa, polisi wamewaruhusu waandishi wa habari 10 kuingia na baadhi ya ndugu wa watuhumiwa. Hata hivyo imeelezwa kwamba walioingia mahakamani humo wametakiwa kuacha simu zao nje.

Mashahidi wanaotakiwa kutoa ushahidi wao leo ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai.

Send this to a friend