Polisi wafunga akaunti za benki za Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu

0
41

Jeshi la Polisi limefunga akaunti zote za Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) katika Benki ya CRDB hatua iliyopelekea mtandao huo kusitisha kwa muda shughuli zake nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya THRDC, Polisi wamekiri kufunga akaunti hizo ili kuweza kulifanyia kazi suala lililopo mbele yao. Jeshi hilo limesemea kuwa mtandao huo haijawasilisha mikataba kati yake na wafadhili katika Ofisi za Hazina na Ofisi za Msajili.

Kikao cha dharura cha Bodi ya Wakurugenzi ya mtandao huo kimemamua kusitisha shughuli zake kwa muda ili kupata muda wa kushughulikia tatizo lililopo mbele yao.

Kwa mujibu wa Vicky Ntetema ambaye ni mwenyekiti wa bodi amesema Mratibu wa THRDC aliyeitwa Makao Makuu ya Polisi kwa ajili ya mahojiano ameachiwa kwa dhamana ya TZS 200 milioni.

Send this to a friend