Polisi walaumu panya kwa kula 200kg za bangi za ushahidi

0
32

Polisi nchini India wamewalaumu panya kwa kuharibu karibu kilo 200 za bangi iliyonaswa kutoka kwa wahalifu na kuhifadhiwa katika vituo vya polisi kama ushahidi.

Jaji Sanjay Chaudhary amesema kwamba mahakama ilipowataka polisi watoe dawa hizo iliyokamatwa kama ushahidi, waliiambia mahakama kuwa kilo 195 za bangi ziliharibiwa na panya.

Taarifa iliyosomwa mahakamani ilisema: “Panya ni wanyama wadogo na hawana hofu na polisi. Ni vigumu kulinda bangi hiyo kutoka kwao.”

Katika kesi nyingine inayohusu kilo 386 za bangi, polisi waliwasilisha ripoti yao mahakamani wakisema baadhi ya bangi hiyo ililiwa na panya.

Hakimu Chaudhary aliiambia mahakama kuwa takriban kilo 700 za bangi zilizonaswa na polisi zilikuwa zimehifadhiwa katika vituo vya polisi wilayani Mathura na kwamba “zote zilikuwa katika hatari ya kushambuliwa na panya.”

Mnamo 2018, maafisa wanane wa polisi wa nchini Argentina walifukuzwa kazi baada ya kuwalaumu panya kwa kutoweka kwa nusu tani ya bangi kutoka kwenya ghala la polisi.

Lakini wataalamu walipinga madai hayo, wakisema kwamba wanyama hao hawakuweza kumaliza kiasi hicho kama chakula kwa kuwa kama wangekula, maiti nyingi zingepatikana kwenye ghala.

Send this to a friend