Polisi wamkamata mwanaume aliyeonekana akiwatishia watu kwa silaha

0
22

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Derick Derick Junior (36), mkazi wa Salasala, Kinondoni ambaye picha mjongeo (video) zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii akitishia watu kwa silaha.

Taarifa iliyotolewa na Polisi imesema uchunguzi umebaini tukio hilo lilitokea Oktoba 27, mwaka huu saa 12:30 asubuhi maeneo ya Masaki ‘1245 night club’ Kinondoni ambapo mtuhumiwa alimjeruhi Julian Bujuru sehemu ya jicho na pua kwa kumpiga na kitako cha bastola.

“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka linakamilisha utaratibu wa kisheria ili mtuhumiwa aweze kufikishwa katika vyombo vingine vya sheria haraka iwezekanavyo,” imeeleza taarifa.

BAKWATA yakanusha taarifa ya Polisi juu ya mtuhumiwa wa ubakaji

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuwa halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote anayemiliki silaha, atakayebainika kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na sheria, kanuni na taratibu zilizoainishwa katika kibali chake cha kumiliki silaha.