Polisi wamsaka kijana anayedaiwa kuua ndugu zake Kenya

0
92

Polisi wa Ol Kalou nchini Kenya wanamsaka kijana mwenye umri wa miaka 27 anayetuhumiwa kuwaua ndugu zake na kuwajeruhi watoto wawili kwa kisu katika eneo la Mundi Estate, usiku wa Alhamisi.

Kamanda wa Polisi wa Nyandarua Central, Samuel Kamau, amesema mtuhumiwa alimuua dada yake mwenye miaka 29 papo hapo, kisha kumjeruhi vibaya mdogo wake wa kiume mwenye miaka 9 ambaye alifariki alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya JM Kariuki.

Katika tukio hilo lililotokea majira ya saa mbili usiku, mtuhumiwa pia aliwajeruhi watoto wengine wawili ambapo mmoja alitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani, huku mwingine akiendelea kupokea matibabu hospitalini.

Polisi wamesema bado haijulikani sababu ya shambulio hilo la kikatili.

Send this to a friend