Polisi wamshikilia aliyemkata kichwa mtoto wake

0
46

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia mtu mmoja aitwaye Amedius Mfoi (25) dereva bodaboda mkazi wa Muriet Jijini Arusha kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake aitwaye Amani Amedius Mfoi (03) Mkazi wa Morombo jijini Arusha.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, kamishna msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 23, 2024 saa 12:00 jioni mtaa wa Murieti Tarafa ya Elerai katika manisipaa ya jiji la Arusha, ambapo alimkata shingo mtoto huyo na kitu chenye ncha kali na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

“Baada ya taarifa hizo kufika, Jeshi la Polisi mara moja tulianza uchunguzi na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kushirikiana na wananchi, na uchunguzi wa shauri hilo unaendelea,” ameeleza.

ACP Masejo ameongeza kuwa baada ya uchunguzi kukamilika jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Send this to a friend