Polisi: Wanaodai kutishiwa maisha walete ushahidi

0
52

Jeshi la Polisi limesema endapo kuna mtu yeyote ametishiwa maisha kutokana na sababu mbalimbali, afike kituo cha polisi ili awasilishe ushahidi alionao kwa ajili ya uchunguzi ikiwemo kuwakamata wahusika.

Wito huo umetolewa kufuatia baadhi ya watu kujitokeza kwenye mitandao ya kijamii na kudai wametishiwa maisha kwa sababu mbalimbali, jambo ambalo jeshi la polisi limedai linawajengea wananchi hofu na maswali yasiyo na msingi.

Aidha, Jeshi la Polisi limekemea tabia ya baadhi ya watu wanaojitokeza na kuzusha habari zisizo na ukweli kuhusu kutishiwa maisha yao kwa nia ya kuleta taharuki kwa wananchi.

Madereva Kenya wakimbilia Tanzania kununua mafuta kwa bei nafuu

“Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wale wachache wanaoendeleza mtindo ambao si wa kisheria, kutoa taarifa zenye nia ya kuzusha na kuwajengea hofu wananchi kuacha tabia hiyo, na abadala yake wafuate taratibu za kisheria ikiwemo kutoa taarifa vituo vya polisi,” imesema.

Send this to a friend