Polisi waruhusu maandamano ya CHADEMA

0
43

Jeshi la Polisi limeruhusu kufanyika maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kesho Januari 24, 2024, huku likieleza kuwa maandamano hayo hayatazuiwa iwapo hayataleta uvunjifu wa amani au kusababisha kutendeka kwa vitendo vya kiuhalifu.

Katika taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi, imetoa rai kwa viongozi wa CHADEMA na wanachama kuzuia lugha za uchochezi na kejeli zinazoweza kupelekea kutendeka kwa vitendo vya uvunjaji wa sheria.

“Mtalazimika kufuata utaratibu wa kisheria katika maeneo yote kwa kadri mtakavyoelekezwa na wasimamizi wa sheria, polisi wakiwa ni kiongozi katika eneo hilo mlilolitolea taarifa,” imesema taarifa.

Taarifa imeongeza kuwa maandamano hayo yasisababishe uvunjifu wa amani au watu kuibiwa au kuporwa na yawe katika zilizokubaliwa ikiwani pamoja na kutoanzishwa kwa mambo mengine ambayo hayamo kwenye taarifa iliyotolewa polisi.

Send this to a friend