Polisi washikiliwa kwa kuuza pombe haramu na kuua watu 17

0
33

Katika kisa kilichoshangaza katika eneo la Kirinyaga nchini Kenya, watu 17 wamepoteza maisha baada ya kunywa pombe haramu ambayo inadaiwa waliuziwa na maafisa wa polisi.

Tukio hilo limetokea baada ya maafisa hao kudaiwa kuvunja ghala la polisi na kuiba kileo hicho kilichokuwa kimewekwa kama ushahidi mahakamani.

Mmoja wa washukiwa wa kesi hiyo ni aliyekuwa Afisa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kiamaciri, Kennedy Mugambi, ambaye kwa sasa anashikilia nafasi ya Mkuu wa Uendeshaji wa Operesheni (SOP) pamoja na washirika wake, Allan Kiamazi, Brian Kariuki, na Francis Muteithia ambao wote wanadaiwa kuhusika katika wizi huo.

Madagascar yapitisha sheria ya kuwahasi wabakaji wa watoto

Baada ya kuiba pombe hiyo, washukiwa hao wanadaiwa kuiuza kwa mfanyabiashara wa ndani ambaye aliiuza katika baa moja huko Kangai kwa Ksh.20,000 na ndipo watu 17 walipopoteza maisha yao baada ya kuuziwa pombe hiyo.

Mmiliki wa baa hiyo, John Muriithi Karaya, tayari amefikishwa mahakamani na kwa sasa anashikiliwa yeye pamoja na maafisa hao huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Send this to a friend