Polisi wathibitisha kuwashikilia Mwabukusi na Mdude, msako unaendelea

0
32

Baada ya taarifa iliyotolewa Agosti 11, 2023 na Jeshi la Polisi likiwaonya wanaofanya uchochezi kwa lengo la kuiangusha Serikali, Jeshi limetangaza kuwakamata watu wawili wanaodaiwa kuhusika kufanya vitendo hivyo.

Watu hao waliokamatwa ni Boniphace Anyasile Mwabukusi na Mpaluka Said Nyagali maarufu kama ‘Mdude’ na mahojiano zaidi na watuhumiwa hao yanaendelea.

Jeshi la Polisi limesema watuhumiwa hao walikamatwa usiku wa kuamkia Agosti 12 mwaka huu katika eneo la Mikumi mkoani Morogoro.

Aidha, limesema linaendelea kuwafuatilia na kuwakamata watuhumiwa zaidi walioandaa na kutoa maneno ya uchochezi, kazi inayoendelea kufanyika kwa mujibu wa sheria.

Send this to a friend