Polisi wavunja ‘uti wa mgongo’ wa Panya Road

0
62

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema kwa mkoa huo upo Sshwari kufuata operesheni kabambe ya kuwakamata Panya Road waliokuwa wakifanya matukio ya uhalifi maeneo mbalimbali.

Makalla amesema mpaka sasa operesheni imefanikiwa kuwafikisha mahakama watuhumiwa 35 na wengine 17 wanaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Kutokana na hilo amewatoa hofu wananchi wa mkoa huo na kulipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya kuvunja uti wa mgongo wa mtandao mzima wa Panya Road.

Ili kuhakikisha matukio kama hayo hayajirudii mara kwa mara, Makalla amesema wameweka mpango mkakati endelevu kwa kudhibiti uhalifu wa aina yoyote usitokee kwenye mkoa huo.

Send this to a friend