Polisi wawaonya ‘bodaboda’ kuingilia misafara ya viongozi

0
26

Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Kigoma kimekemea tabia za madereva wa pikipiki zinazobeba abiria, maarufu ‘bodaboda’ kuingilia misafara ya viongozi na wakati mwingine kuwa mbele ya misafara hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo, Ibrahim Mbaruku wakati wa mkutano wa pamoja baina ya madereva pikipiki, bajaji na Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Kigoma.

Amesema bodaboda hao wamekuwa wakiingilia misafara ya mawaziri, mkuu wa mkoa na misafara mingine ya viongozi pasipokuchukua tahadhari ya kusababisha ajali ikiwa ni pamoja na watumiaji wengine wa barabara.

Mbaruku amesema polisi imejidhatiti kuhakikisha inawashughulikia bodaboda wanaovunja sheria na taratibu za usalama barabarani ikiwemo kubeba mishikaki, kutovaa kofia ngumu, kung’oa vioo vya pembeni ‘side mirror’ na kuweka majina yao kwenye namba ya usajili bila kufuata taratibu.

Send this to a friend