Polisi wawasaka wazazi wa mwanafunzi aliyeolewa

0
49

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limesema linaendelea kuwasaka wazazi wa mwanafunzi Rachel Fungai ambaye sherehe ya ndoa yake ilizuiwa baada ya kuolewa wakati tayari amechaguliwa kujiunga na kidato cha tano.

Kamanda Polisi mkoani humo, ACP Janeth Magomi amesema watuhumiwa hao wanaendelea kusakwa baada ya kushindwa kujisalimisha kama walivyoagizwa na Jeshi la Polisi.

“Tuliwakamata watuhumiwa wanne akiwemo yule muoaji pamoja na ndugu wa yule binti aliyekuwa anaozeshwa, wale wote wamepewa dhamana, yule binti tunaendelea kumhifadhi kwa maana ya ulinzi wake lakini wakati huo tunaendelea na upelelezi ili tufikishe jalada kwa mwanasheria wa Serikali na sheria iweze kuchukua mkondo wake,” amesema.

Waziri Mkenda afafanua utaratibu wa ufanyaji mitihani kwa walimu

ACP Magomi amesema binti huyo alitolewa mahari ya ng’ombe kati ya 14 na 15 ili aweze kuolewa na mwanaume huyo wakati ambapo amechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule moja wapo ndani ya mkoa huo.

Send this to a friend