
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji limesema linamshikilia Winfrida Malembeka, na kwamba hajatekwa kama inavyodaiwa.
Winfrida anashikiliwa kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uchochezi, kuhamasisha vurugu na maandamano Desemba 09, 2025, kupitia mitandao ya kijamii akishirikiana na watu wengine.
Aidha, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kujiepusha na uchapishaji na usambazaji wa taarifa za kichochezi zenye kuleta taharuki kwa jamii kwani halitasita kuchukua hatua za kisheria.






