Polisi yakanusha kuwashikiliwa vijana kwa siku 26 bila kuwapa dhamana

0
111

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji limekanusha taarifa ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu iliyotolewa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza kuwa vijana wanaoshikiliwa kwa siku 26 katika kituo cha Polisi Mkuranga wamepewa dhamana.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema walifuatilia kwa kina taarifa hiyo katika kituo cha Polisi Mkuranga ambapo katika ufuatiliaji huo, hakuna kumbukumbu zinazoonesha watuhumiwa hao wanne walishikiliwa na kunyimwa dhamana.

“Hakuna kumbukumbu zinazoonesha watuhumiwa wanne wanaoshikiliwa bila kupewa dhamana au kufikishwa mahakamani kwa siku 26, na hakuna mtuhumiwa yeyote anayekabiliwa na kosa lisilo dhaminika katika kituo hicho cha Polisi Mkuranga,” imesema.

Aidha, jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kuimarisha mfumo wa haki jinai ikiwa ni pamoja na kuwaomba wananchi kufuata sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kutosambaza taarifa za uongo.

Send this to a friend