Polisi yakanusha watu kuondolewa figo na watu wanaojifanya machinga

0
47

Jeshi la Polisi limekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu watu wanaojifanya machinga wanaouza manukato mitaani, kuwalewesha watu kupitia manukato kisha kuwatoa figo zao, ikisema hakuna tukio kama hilo ambalo limeripotiwa eneo lolote nchini.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, imesema ujumbe huo unaosambaa umeambatanishwa na picha mjongeo (video clip) ambayo imeondolewa sauti, ambapo polisi wamesema wanafanya uchunguzi kujua sababu za aliyeisambaza video hiyo kutoa sauti.

“Kwa vile, Jeshi la Polisi tunayo mashirikiano ya kikanda na majeshi mengine ya Polisi tutawashirikisha ili kupata chanzo cha picha hiyo mjongeo ni nini, ni tukio gani na limetokea wapi,” imeeleza taatifa hiyo.

Aidha, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wanaoendelea kusambaza au aliyenayo video hiyo, wasiendelee kuisambaza.

Send this to a friend