Polisi yawashikilia watoto waliovunja vioo vya SGR kwa mawe

0
35

Jeshi la Polisi limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kuvunja vioo viwili vya treni ya Reli ya Kisas ya Umeme (SGR) kwa mawe katika Kijiji cha Manase Wilaya ya Chamwino wakati treni hiyo ikipita kutoka Dar es Salaam.

Tarifa ya polisi imesema watuhumiwa hao walifanya uharibifu huo Novemba 22, mwaka huu kwa kurusha mawe kwa pamoja ili kuona mawe waliyorusha yataweza kushindana na kasi ya treni.

Aidha, limesema baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifanya msako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa ambao mmoja ana miaka 16 na mwingine umri wa miaka 12, wote wakazi wakazi wa Kijiji hicho.

Mbali na hayo, Jeshi la Polisi limetoa rai kwa wazazi na walezi kuzingatia malezi kwa familia ili kuacha vitendo ambavyo vitasababisha uharibu kwenye reli, kwani vinakinzana na sheria za nchi.

Send this to a friend