Precision Air yaanza taratibu za kuwalipa waathirika wa ajali

0
43

Mkurugenzi wa Shirika la Precision Air, Patrick Mwanri amesema mchakato wa kuwalipa fidia familia za waathirika wa ajali ya ndege iliyotokea Bukoba mkoani Kagera tayari umeanza.

Akizungunza na waandishi wa habari leo Novemba 14, 2022 jijini Dar es Salaam amesema mchakato huo hautowekwa hadharani na utafanyika kwa umakini mkubwa kwa mujibu wa taratibu uliowekwa.

“Shirika letu lina bima na ipo kulingana na taratibu za uendeshaji mashirika ya ndege. Hivi ninavyoongea taratibu zile zimeshaanza na wahusika tumeshaanza kuwasiliana nao ili waweze kupata taarifa rasmi ya nini kinahitajika,” amesema.

Walioshirikiana na Majaliwa kuokoa abiria wa ajali ya ndege waomba mafunzo

Aidha, Shirika hilo limemshukuru Rais Samia na Serikali kwa ujumla kwa kuendelea kushirikiana nao pamoja na wavuvi waliojitokeza kutoa msaada kwa abiria wa ajali hiyo.

Hivi karibuni Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Bagayo Saqware alitaja kiwango cha fidia kwa waathirika wa ajali hiyo kuwa ni takribani TZS bilioni 396 na fidia ya TZS bilioni 116 kwa shirika la Precision Air.

Ndege ya Precision Air ilipata ajali Novemba O6, mwaka huu katika Ziwa Victoria Bukoba mkoani Kagera na kuua watu 19, huku watu 24 wakifanikiwa kuokolewa.

 

Send this to a friend