Prof. Assad: Wengi wanaozungumzia bandari si wataalamu wa uwekezaji

0
40

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Prof. Mussa Assad amesema tatizo lililopo katika suala la ushirikiano wa Tanzania na Dubai kwenye uendeshaji wa bandari ni kuwasikiliza wanasheria ambao hawana utaalamu wa masuala ya uwekezaji.

Amesema hayo wakati wa mahojiano na kituo cha Channel Ten ambapo amebainisha kuwa suala la uwekezaji wa bandari nchini linatafsiriwa visivyo kutokana na usomaji mbaya wa sheria na kutokuwa na utaalamu na masuala ya uwekezaji.

“Tatizo ni usomaji mbaya, watu si wataalamu wa uwekezaji. Kipengele kinachozungumziwa pale ni land rights (haki za ardhi) haki ya ardhi sio umiliki, ni utumiaji wa ile ardhi, yaani haki ya kutumia na kupata access. Kwa mfano Bandari ya Dar es Salaam mmiliki ni Shirika la Bandari, na ana hati, kwahiyo atampa huyu mtu haki ya kutumia, hawezi kuwa anamiliki, atapata haki ya matumizi tu,” amesema.

Akizungumzia kuhusu suala la ukomo wa mkataba huo amesema hayo ni makubaliano kati ya nchi na nchi, hivyo ukomo utapatikana katika mikataba ya miradi ambayo itakwenda kutekelezwa.

“Kwa sababu watu wamelipigia kelele jambo hili, si tatizo kubwa sana kuweka ukomo, unaweza kuweka miaka 25, 30 basi halafu watu wakafurahi kwamba ukomo umewekwa, lakini muhimu ni ile mikataba ya chini, ile ni mikataba inayotekelezeka ndiyo inayoweza kuwa na ukomo, lakini mkataba wa nchi na nchi si lazima uwe na ukomo. Na hata mikataba ya nchi zingine ndivyo inavyokuwa,” ameeleza.

Kinana: Wapinzani jengeni hoja na si kumkejeli Rais

Ameongeza kuwa bara la Afrika linahitaji wawekezaji kutoka nje ili kusaidia kukabiliana na changamoto zinazozikumba bandari zake, huku akitaja changamoto hizo kuwa ni maabadiliko ya teknolojia na mifumo, wafanyakazi katika ngazi za kati na ngazi za juu kutokuwa na ujuzi unaotakiwa na kutokuwa na mitaji ya kutosha kuwekeza zaidi bandarini.

Send this to a friend