Prof. Janabi aeleza utaratibu wa kufuatwa familia ya Mshale ipewe mwili wa marehemu

0
38

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohammed Janabi ameitaka familia ya marehemu Swalehe Mshale (74) kufika katika uongozi wa hospitali hiyo ili kukamilisha taratibu za kupatiwa mwili wa mpendwa wao.

Tamko hilo ni kufuatia familia ya marehemu kuiomba Serikali kuwafutia deni la milioni 10 wanalodaiwa na hospitali ya Muhimbili ambalo limefanya wasiruhusiwe kuchukua mwili wa mpendwa wao toka alipofariki Februari 10, mwaka huu.

Precision Air: Ndege haikufika Dodoma, kulikuwa na tatizo la injini

“Utaratibu upo very clear ni kurudi hapo kwa watu wa social (Ustawi) kuna barua ambayo wanatakiwa kuandika ya ‘commitment’ wataacha ID (kitambulisho) wataruhusiwa kuchukua mwili halafu baada ya hapo watakuwa na makubaliano kama ni miezi sita, kama ni mwaka kila mtu anaji-commit kivyake kwamba atakuwa analipa kidogokidogo, hivyo wakamuone Mkurugenzi wa Uuguzi,” amesema Prof. Janabi.

Ameongeza, “tatizo ni kwamba watu wa namna hii hawafuati taratibu wanazotakiwa kuzifuata, badala yake wanakimbilia kwenye jamii wakitarajia tutapata pressure, ‘we don’t get pressure’, hizi hela ni za Serikali.”

Send this to a friend