Prof Kabudi: Serikali haijazuia mikutano ya hadhara ya kisiasa

0
45

Waziri wa Katiba na Sheria  Prof. Palamagamba Kabudi amesema mikutano ya kisiasa nchini haijazuliwa, bali inaratibiwa na imewekewa utaratibu wa kufanyika.

Kabudi amesema hayo jijini Dodoma akiwasilisha mafanikio ya wizara hiyo kwa miaka 60, na kueleza kwamba mambo yote yanayofanyika nchini, lazima yazingatiame sheria na miongozo mingine.

“Hakuna jambo lolote ambalo linafanyika bila utaratibu. Wengi tunaisoma sura ya pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya haki za binadamu bila ya kosoma ibara ya 30, imeweka mipaka katika kufaidi uhuru wako,” amesema Kabudi.

Akizungumzia suala la umri wa msichana kuolewa amesema bado wanaendelea mashauriano na wadau mbalimbali kwa maelekezo ya Bunge ili waone njia nzuri ya kutekekeza maombi au mahitaji ya umri wa mtoto wa kike kuolewa uwe ni miaka 18.

“Tumeandaa muswada na kuupeleka bungeni, kamati ya bunge kupitia muswada huo imeiachia serikali iendelee na mashauriano na wadau mbalimbali kwa hiyo sasa tunaendelea mashauriano na wadau mbalimbali kwa maelekezo ya Bunge ili baadaye tuone njia nzuri zaidi ya kutekeleza maombi au mahitaji ya umri wa mtoto wa kike kuolewa iwe umri wa miaka 18,” amesema.

Kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili, Kabudi amesema mpaka sasa wizara hiyo imefanikiwa kutafsiri sheria 154 na kuzipeleka katika lugha ya hiyo, huku akisema kuwa kazi hiyo bado inaendelea.

Send this to a friend