Prof. Lipumba amdai IGP Sirro saa yake

0
51

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro kuitafuta saa yake ya mkononi aliyonyang’anywa na askari wake wakati wa mvutano ulioibuka karibuni.

Akizungumza na wanachama wa chama hicho na wananchi mkoani Tabora Lipumba amelishutumu jeshi hilo kwa kuvuruga shughuli za chama hicho zilizopangwa kufanyika, ikiwemo uziunduzi wa mashina katika kata za Mbugani na Mapambano pamoja na kuchangia damu. Amesema polisi waliwazuia kufanyia shughuli hiyo kwenye ofisi zao, badala yake wafanyie kwenye ukumbi, na kwamba mwishoni walifanikiwa kuchangia chupa 20.

Amesema atamshauri Rais atembee kwenye kauli zake za kutetea demokrasia ya kweli, yenye msingi wa maendeleo pamoja na kulinda heshima na utu wa Watanzania.

Ameongeza kuwa haki ni muhimu kwani itawezesha wananchi kufanya kazi kwa uhuru, hivyo kujiletea maendeleo na kwamba Rais atakumbukwa na kujipatia heshima kutokana na kusimamia kauli yake, na kwamba akija kugombea tena kazi inakuwa nyepesi.

 

Send this to a friend