Prof. Mkenda: Elimu inayotolewa imwandae mhitimu kujiajiri na kuajiriwa

0
43

Waziri wa Elimu, Syansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amewaagiza Baraza la Elimu ya Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kuhakikisha wanasimamia mahudhui yanayotolewa katika vyuo ili kuongeza ubora wa elimu na ujuzi.

Amebainisha hayo wakati akifunga maonesho ya elimu ya sayansi na mafunzo ya ufundi stadi TVET yaliyofanyika jijini Dodoma.

“Rais Samia wakati akihutubia bunge, aliagiza Wizara ya Elimu kupitia sera na mitaala ya elimu ili kuongeza ubora wa elimu, kuhakikisha elimu inayotolewa inaleta ujuzi ili kumwandaa mhitimu kumudu mazingira na aweze kuajiriwa na kujiajiri” amesema.

Aidha Prof. Mkenda amesema katika kuhakikisha zoezi la kutoa mikopo katika vyuo vya kati na ufundi linafanyika kwa ufasaha, inahitajika kuwa na takwimu mahususi za vyuo vyote vinavyotoa mafunzo nchini.

“Tukiwa na takwimu sahihi tukajua ni kozi gani ambazo wanafunzi wakisoma wanaajiriwa kwa haraka tunaweza kuongea na benki zetu wakatoa mikopo kwa wanafunzi hao na watarejesha wenyewe watakapo ajiriwa” ameeleza.

Send this to a friend