Prof. Mkenda: Ukihitimu kidato cha nne utapokea vyeti viwili

0
63

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema katika mtaala mpya, elimu ya sekondari itakuwa na mikondo miwili ambayo ni elimu jumla na elimu ya amali (mafunzo ya kazi) ambapo mwanafunzi atatakiwa kuchagua moja ya mkondo atakaosoma.

Profesa Mkenda amesema elimu ya amali itakuwa na michepuo kadhaa ambayo masomo ya darasani yatakuwa ni machache zaidi, na iwapo mwanafunzi atamaliza kidato cha nne atapatiwa vyeti viwili kimoja kikiwa cha kuhitimu elimu ya kidato cha nne na kingine kinachoonesha masomo ya amali aliyofuzu kama kilivyo cheti cha VETA.

“Kwa mfano umeenda kujifunza ufundi magari kwa maana ya ufundi uhandisi utapata cheti cha form four na cheti cha kukuruhusu kuajiriwa serikalini ama ukaajiriwa na kampuni na kadhalika,” ameeleza.

Ameongeza kuwa mwanafunzi atakapomaliza kidato cha nne endapo atakuwa katika mkondo wa mafunzo ya amali, anaweza kutumia masomo machache ya darasani kwenda kidato cha tano na sita.

Send this to a friend