Prof. Mkumbo: Watumishi wa umma zingatieni nidhamu kazini

0
7

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu ili lengo la kuwatumikia wananchi litimie ipasavyo.

Prof. Kitila ameyasema hayo katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mkoani Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa weledi huo unaweza kufikiwa ikiwa watumishi hao watakuwa na utamaduni wa kujifunza masuala mbalimbali yanayoihusu wizara, kufanya kazi kwa bidiii, na kuzingatia sheria, taratibu na kanuni.

“Wizara yetu kwa kweli ni Wizara mtambuka, siyo wizara ya kisekta kwahiyo mnapaswa kufahamu mambo ya karibu kila sekta katika nchi hii. Kwahiyo huwezi kusema mimi madini hayanihusu, nishati au kilimo hakinihusu, hapana. Hii wizara ni mtambuka, na tunatarajiwa wote tujifunze”, ameeleza Prof. Kitila.

Amesema kuwa weledi hufanya mchango wa mtumishi katika taasisi kuonekana muhimu zaidi pengine kuliko mtumishi mwingine hivyo amewahimiza watumishi hao kuupa weledi kipaumbele.

Aidha amelitaka Baraza hilo kujenga utamaduni wa uwazi, mijadala na majadiliano akibainisha kuwa vitu hivyo ndivyo vyenye kuakisi lengo la Baraza la Wafanyakazi sehemu za kazi.

 

Send this to a friend