Prof. Ndalichako: Wanafunzi wasilipishwe ada kwa kipindi walichokua majumbani

0
43

Serikali imesema kuwa wanafunzi hawatolazimika kulipa ada ya kipindi walichokuwa majumbani kutokana na shule hizo kufungwa na serikali kama njia ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Hayo yamesema na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichoka ambaye ameeleza kuwa wanafunzi kabla ya kurejea majumbani walikuwa tayari wamelipa ada, hivyo wanaporejea shule wataendelea kutumia fedha zile zile, na hakutakuwa na malipo mapya.

“Wanafunzi walikuwa wameshalipa ada kabla ya kufunga shule, wanaenda kuendelea pale pale walipoachia, hakuna malipo ya ziada,” amesema Ndalichako

Amezionya shule zinazotaka kutumia corona kama kitega uchumi, huku akisema kuwa wizara haitosita kuchukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kuzifutia usajili shule hizo.

Hata hivyo amewataka wanafunzi ambao hawakuwa wamemalizia ada zao kufanya hivyo ili kuziwezesha shule kujiendesha.

Msikilize hapa chini akitoa maelekezo zaidi;

Send this to a friend