Prof. Shukrani Manya ateuliwa kuwa Naibu Waziri wa Madini

0
58

Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli amemteua Prof. Shukrani Manya kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Prof. Manya pia ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Manya alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania.

Uteuzi wa Prof. Manya unaanza leo Disemba 11, 2020 na ataapishwa leo mchana Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma.

Send this to a friend