Programu ya “Learning for Life” ya Serengeti Breweries yawanufaisha vijana

0
40

Programu ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti Breweries Limited ya kuwawezesha zaidi ya vijana 400 Hanang kupitia stadi muhimu na maarifa kwa ajili ya maendeleo yao, ujuzi wa kibiashara, usimamizi wa fedha, na mipango bora ya biashara.

Mafunzo hayo ya siku 3 yamekamilika na yametimiza lengo lake la kutoa Mafunzo ambayo yamewaandaa vijana na stadi za kujiajiri na kujenga fursa za kazi. lengo kuu la Serengeti Breweries Limited ni kuwasaidia kutambua fursa na kuzitumia ipasavyo. Programu hiyo iliwakutanisha na wa kutengeneza mtandao wa watu wa ujuzi mbalimbali , kujifunza kutoka kwa wataalamu, na kupata ufahamu wa vitendo kutoka sekta tofauti, yote kwa lengo la kupunguza ukosefu wa ajira, kupunguza umaskini, na kujenga mustakabali ulio bora kwa vijana wa Wilaya ya Hanang.

Send this to a friend