PUMA ENERGY TANZANIA YAANDAA FUTARI KWA LENGO LA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA UMOJA

Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeandaa futari maalum kwa wateja na washirika wake ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuimarisha mahusiano na kuonesha shukrani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mkusanyiko huo umewaleta pamoja wateja, wadau na uongozi wa kampuni katika hali ya umoja, tafakari na malengo ya pamoja.

Futari hiyo iliandaliwa kama ishara ya kuthamini wateja ambao ushirikiano wao wa muda mrefu una mchango muhimu katika shughuli za kampuni kote nchini. Kwa kukutana nje ya mazingira rasmi ya biashara, Puma Energy ililenga kutambua mchango wa wateja wake na kuimarisha mahusiano yaliyojengwa juu ya imani na heshima ya pande zote.

Ikiwa imefanyika katika mwezi wa Ramadhani mwezi unaosisitiza huruma, ukarimu na mshikamano, chakula hicho cha pamoja kilitoa fursa ya mazungumzo yasiyo rasmi na kujenga ukaribu wa kibinafsi. Wageni walifuturu pamoja na kushirikiana moja kwa moja na wawakilishi wa kampuni, jambo lililoimarisha uhusiano zaidi ya ule wa kila siku ambao huhusisha biashara. Tukio hilo limeakisi mtazamo wa kampuni kwamba ukuaji endelevu haujengwi tu katika misingi ya kibiashara bali kwa ushirikiano wa kudumu.
“Mkusanyiko huu ni njia yetu ya kutambua umuhimu wa wadau na jamii katika safari yetu,” amesema Bi. Fatma M. Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania. “Imani yenu endelevu inatuwezesha kufanya kazi kwa uwajibikaji na kupanua upatikanaji wa suluhisho za nishati zenye kuaminika. Ramadhani ni wakati muhimu wa kuonyesha shukrani na kuthibitisha upya dhamira yetu ya kutoa huduma kwa uadilifu na ushirikiano,” aliongeza.

Katika tukio hilo Sheikh Mkowe Abdallah alisisitiza umuhimu wa jamii na wajibu wa pamoja katika kipindi cha Ramadhani. “Kukutana pamoja kwa ajili ya futari huimarisha vifungo vya urafiki na heshima ya pande zote. Ni wakati wa kutafakari wajibu wetu kwa kila mmoja na kwa jamii pana, na kutenda kwa uadilifu na huruma,” alisema Sheikh Mkowe Abdallah.
Wakati jioni hiyo ikilenga shukrani na umoja, Puma Energy inaendelea kupanua suluhisho zake za nishati mbadala nchini Tanzania. Kituo kikuu cha CNG (gesi asilia iliyoshindiliwa) kilichozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam kinachotajwa kuwa miongoni mwa vikubwa zaidi barani Afrika kinasambaza gesi kwa vituo vidogo vya CNG kote nchini, na hivyo kuongeza upatikanaji wa mafuta safi na nafuu kwa magari, mabasi na malori. Mtandao unaokua wa CNG unaunga mkono juhudi za kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala zinazolinda mazingira na kuboresha upatikanaji wa mafuta kwa biashara na jamii.

Uwekezaji huo wa CNG pia umechangia shughuli za kiuchumi za ndani. Wakati wa ujenzi, mradi huo ajira zaidi ya 300 zilipatikana, zikiwemo nafasi maalum kwa wahandisi na mafundi stadi, huku ukishirikisha wakandarasi wa ndani pamoja na biashara ndogo na za kati. Kwa kupanua upatikanaji wa gesi asilia kama mafuta mbadala ni jambo linalounga unaunga mkono malengo mapana ya Tanzania ya kuwa na nishati mseto na maendeleo endelevu.

Kwa kuhitimisha, kampuni ya puma imesisitiza umuhimu mpana wa mikusanyiko ya aina hii kuwa zaidi ya tukio lenyewe. Emmanuel G. Bakilana, Mkuu wa Idara ya Sheria na Mahusiano ya Kampuni wa Puma Energy Tanzania, amesema: “Matukio kama futari hii hutupa fursa ya kutafakari wajibu wetu wa pamoja kwa wateja na jamii. Ni wakati wa kuwashukuru wanaounga mkono shughuli zetu na kuimarisha misingi ya biashara yenye maadili na ushirikiano inayotuongoza kila siku.”

Kupitia futari hii pamoja na uwekezaji wake endelevu katika miundombinu ya nishati, Puma Energy Tanzania imethibitisha tena dhamira yake ya kujenga ushirikiano wa kudumu na wateja na wadau wake huku ikichangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
Kuhusu Puma Energy
Puma Energy ni kampuni inayoongoza duniani katika biashara ya nishati ya mkondo wa chini (downstream), ikitoa huduma za nishati kwa usalama katika zaidi ya nchi 35, hususan Amerika ya Kati na Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara. Shughuli zake za mkondo wa chini zinajumuisha mafuta, huduma za anga (aviation), vilainishi (lubricants), gesi ya LPG na lami (bitumen). Dhamira ya kampuni ni kuwezesha jamii kwa nishati ili kuchochea ukuaji na ustawi kwa kuhudumia kwa njia endelevu mahitaji ya wateja katika nchi zenye fursa kubwa duniani.
Kwa maelezo zaidi tembelea: www.pumaenergy.com








