Putin ampa uraia wa Urusi aliyevujisha taarifa za siri za Marekani

0
36

• Edward Snowden apewa uraia wa Urusi baada ya kuvujisha taarifa za siri za Shirika la Usalama la Taifa nchini Marekani.

• Inadaiwa hati nyingi zilizovuja zilihusiana na mipango ya kijeshi, ulinzi na kijasusi zenye maslahi makubwa kwa wapinzani wa Marekani.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametia saini amri ya kumpa uraia wa Urusi Edward Snowden, mshauri wa zamani wa masuala ya usalama ambaye alikimbia Marekani baada ya kuvujisha taarifa za siri kuhusu Shirika la Usalama wa Taifa mwaka 2013.

Snowden ambaye alikuwa akifanya kazi kama mkandarasi mdogo wa NSA (National Security Agency), anatafutwa na mamlaka ya Marekani kwa kusambaza mamia ya hati za siri juu ya programu kadhaa za uchunguzi wa kimataifa zinazofanywa na wakala kwenye baadhi ya vyombo vya habari miaka tisa iliyopita.

Inadaiwa, uvujaji huo ulikuwa kati ya ukiukaji mkubwa zaidi wa usalama katika historia ya Marekani huku akishtakiwa na Idara ya Haki mnamo 2013 kwa kukiuka sheria ya ujasusi ambayo angeweza kukabiliwa na kifungo cha miongo kadhaa jela.

Ripoti ya Kamati ya Ujasusi ya mwaka 2016 ilisema uvujaji huo ulisababisha uharibifu mkubwa kwa usalama wa taifa na kwamba hati nyingi zilizovuja zilihusiana na mipango ya kijeshi, ulinzi na kijasusi yenye maslahi makubwa kwa wapinzani wa Amerika.

Snowden amesema alipanga kuomba uraia wa Urusi tangu mnamo 2020.

Send this to a friend