Rais wa Urusi, Vladimir Putin amekutana na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi na kusema kuwa anataka vita nchini Ukraine imalizike haraka iwezekanavyo.
Putin amesema anaelewa wasiwasi wa New Delhi kuhusu mzozo huo, na kwamba Kyiv ilikataa mazungumzo na kudai kuwa ilikuwa imedhamiria kufikia malengo yake kwenye uwanja huo wa vita.
Makarani 10 wapoteza maisha katika kipindi cha Sensa
“Tutafanya kila kitu kukomesha hili haraka iwezekanavyo. Ni kwa bahati mbaya tu uongozi wa Ukraine ulitangaza kukataa mchakato wa mazungumzo na kusema kwamba unataka kufikia malengo yake kwa njia za kijeshi,” amesema Putin.
Mpaka sasa Urusi inadhibiti karibu theluthi moja ya Ukraine baada ya kutuma vikosi vyake vya kijeshi tangu Februari mwaka huu.