Raia 14 wa Burundi wakamatwa kwa kuingia nchini kinyume cha sheria

0
74

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia wahamiaji haramu 14 raia wa Burundi waliokamatwa wakiwa wameingia nchini kinyume na sheria kwa kutumia usafiri wa magari mawili tofauti ya abiria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa amesema
Katika Kijiji cha Busisi, Tarafa ya Sengerema, jumla ya wahamiaji haramu 13 walikamatwa Novemba 23, 2025 majira ya 7.30 mchana wakiwa wanasafiri ndani ya gari aina ya Tata yenye namba za usajiri T. 337 DYA, mali ya Chiza Francis Lugubi, mkazi wa Dodoma, linalofanya safari zake kati ya Kabanga (Ngara, Kagera) na Mwanza.

Ameongeza kuwa wakati wa kukamatwa, dereva wa gari hilo, aliyetambulika kwa jina la Jonas Richard, alifanikiwa kutoroka eneo la tukio na jitihada za kumsaka zinaendelea.

Watuhumiwa wengine waliohusika katika kuwasafirishaji wahamiaji haramu hao ni pamoja na Mustahper Emily miaka 24, fundi magari na mkazi wa Kahama, Shinyanga na Pendo Matembere miaka 36, kondakta na mkazi wa Nyegezi, Mwanza.

Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema baada ya kuhojiwa, ilibainika kuwa wahamiaji hao waliingia nchini kupitia mpaka wa Kabanga, mkoani Kagera, mnamo tarehe 22 Novemba 2025.

Mtuhumiwa Shadia Japhari Majaliwa, miaka 18, raia wa Burundi na mkazi wa Kisuru, alikamatwa katika eneo la Nyatukara wilayani Sengerema akiwa ndani ya gari aina ya Yutong lenye namba za usajili T 131 DRE.

Send this to a friend