Raia wa China katika mradi wa SGR kizimbani kwa kumpiga mpishi

0
40

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema Jeshi la Polisi linamshikilia mkandarasi wa mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Zheng Yuan Feng raia wa China kwa kosa la kumshambulia mfanyakazi, Lucy Paulo mwenye fani ya upishi katika mradi huo.

TRC imesema Lucy alishambuliwa akiwa jikoni kwa kumtolea lugha chafu na kumpiga, kitendo kilichopelekea kupata majeraha mbalimbali hivyo kupelekwa Hospitali ya Bugando kwa ajili ya kupatiwa matibabu Machi 20 na kuruhusiwa Machi 21,2023

Katika taarifa yake imeeleza kwamba baada ya tukio hilo, Zheng alikamatwa na polisi na kupandishwa kizimbani Machi 24 wilayani Misungwi, na kusomewa mashtaka kwa kosa la kujeruhi na kwamba “kwa sasa yupo rumande katika kituo cha Polisi Misungwi baada ya kushindwa masharti ya dhamana.”

TRC imemtaka mkandarasi ambaye ni kampuni ya CCECC-CRCC kuhakikisha Lucy anapatiwa stahiki zake kwa kufuata sheria, taratibu na kuhakikisha anafanya kazi kwa uhuru wakati wote wa mradi na kueleza kuwa “mkandarasi ameridhia kutekeleza matakwa hayo na TRC itaendelea kufuatilia.”

Send this to a friend